FREDY ERASTO CHAVALA (King Chavala-MC) MWANAHARAKATI WA VIJANA TANZANIA!!!

FREDY ERASTO CHAVALA (King Chavala-MC)

Na huyu ni muasisi wa STAND UP COMEDY TANZANIA, na muanzishaji wa jukwaa la CHRISTIAN STAND UP COMEDY Tanzania,analea vipaji asili na kukuza vilivyoanza kuuzika…ni mkurugenzi wa “LAUGH AGAIN CONCERT SERIES-(LACS)”
Huyu ni Mwanaharakati Mzalendo wa maendeleo ya Vijana na Biashara!
Ni mchekeshaji(Comedian),MC,Mshauri na Mzungumzaji Muhamasishaji (Motivational Speaker),Mwandishi wa vitabu na makala,Blogger, na zaidi ni Mshauri wa Biashara na Utawala kitaaluma(Business and Management Consultant)

Hotline; +255 713 883 797

Advertisements

MIFUKO 600 YA MBOLEA YA RUZUKU YAFISADIWA….WALIOKUFA PIA WAORODHESHWA KUWA WALIGAIWA, KILIMO KWANZA HIKI!!!!!!!!

Delvanus Jeremia (29) aliyechaguliwa kuwa Katibu wa Kamati ya kuandika Majina ya waliogawiwa Vocha za Mbolea Lukunguni Kata ya Kikeo, amejiuzulu.

Jeremia alijiuzulu Ukatibu wa Kamati hiyo hivi karibuni, akidai hayupo tayari kufanya kazi ya kuwaorodhesha wakulima waliopokea mbolea, kutokana na kuwepo tuhuma za Ufisadi.

Alipohojiwa na Mwandishi, Jeremia alithibitisha kuandika barua kwa Mtendaji wa Kijiji hicho, ikiwa ni siku moja baada ya Wakazi wa Lukunguni na Vijiji Jirani kuulalamikia Uongozi wa Kata Kikeo na ule wa Kilimo Mvomero, kuwa umechakachua Mifuko 600 ya mbole ya 2012/2013 na kutishia kutimkia Chadema.

Akifafanua kujiuzulu kwake Jeremia alisema ni kuwepo kwa Maelezo yanayolalamikiwa kwamba baadhi ya viongozi wa Kilimo Mvomero na Kata ya Kikeo, wanashinikiza kuwa wakulima walipata mifuko 450 ya Mbolea ya 2012 na 2013 wakati wananchi wanakataa.

“Sitaki kuhusishwa na Jambo lolote la Vocha za Mbolea kwa sababu kuna malalamiko na manung’uniko ya wakazi wa Lukunguni na vijiji jirani kikiwemo cha Lware tulipofanyia mkutano na viongozi wa Kilimo Wilaya ya Mvomero wakidai hawajapata mbolea hiyo”.alisema.

Aliongeza kuwa, Sababu ya pili ya kujiuzulu ni kuwepo minong’ono na tuhuma ya majina ya waliokufa ambao wamedaiwa kuorodheshwa kuwa wamepata mbolea, jambo ambalo kwa kuwa yeye ni mgeni na ana miezi sita tu, hawezi kuwatambua watu wote.

kwa Hisani ya Habari mseto blog.

Na Joel Nanauka!