Jaji FRANCIS S.K MUTUNGI, MSAJILI MPYA WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA!!!

Image

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemteua Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatatu (Agosti 5, 2013 na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita (Agosti 2, 2013).
Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama na Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu utumizi wa umaa kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi huo Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Tunamtakia kila lakheri katika majukumu yake hayo mapya, ni wazi kuwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini haijakuwa ule msingi wa wananchi kuiamini moja kwa moja maana huonekana kama ni sehemu ya serikali tawala kuwasimamia upinzani zaidi, lakini naamini Msajili mpya atailetea heshima mpya na kuweka misingi huru ya kukuza demokrasia nchini!

Msajili ana kazi moja ya ziada ya kutibu majereha ya mahusiano ya ofisi yake na vyama vya siasa aliyoyaacha msajili mstaafu.

Image

Tunamtakia maisha mema Mheshiwa Tendwa, na utumishi wake utaheshimika tu.

MUNGU IBARIKI OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s