Jaji FRANCIS S.K MUTUNGI, MSAJILI MPYA WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA!!!

Image

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemteua Jaji Francis S.K. Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatatu (Agosti 5, 2013 na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita (Agosti 2, 2013).
Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama na Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu utumizi wa umaa kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi huo Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Tunamtakia kila lakheri katika majukumu yake hayo mapya, ni wazi kuwa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini haijakuwa ule msingi wa wananchi kuiamini moja kwa moja maana huonekana kama ni sehemu ya serikali tawala kuwasimamia upinzani zaidi, lakini naamini Msajili mpya atailetea heshima mpya na kuweka misingi huru ya kukuza demokrasia nchini!

Msajili ana kazi moja ya ziada ya kutibu majereha ya mahusiano ya ofisi yake na vyama vya siasa aliyoyaacha msajili mstaafu.

Image

Tunamtakia maisha mema Mheshiwa Tendwa, na utumishi wake utaheshimika tu.

MUNGU IBARIKI OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

KWA GIA HII…MAENDELEO YETU NI KAMA MAYAI YA POPO!!!

Najivunia sana kuwa Mtanzania, tena mtanzania mzalendo!

Napenda sana maendeleo ya nchi yangu na nafurahia sana juhudi za kweli za serikali za kuleta maendeleo; Najivunia viongozi wanajitoa kwa moyo moyo wote kutimiza majukumu yao ya kila siku, najua ni wachache sana ukilinganisha na wengi ambao wameacha kabisa madili yao ya kazi,wameacha kutumia vichwa vyao ila sasa wanafikiri kwa kutumia tumbo.

Maisha ya mtanzania wa kawaida ni magumu,tena sana,lakini bado hawaachi kuipenda nchi yao naam hata pamaoja na utitiri wa kodi na michango bado watu wanatoa tu bila hiana.

Image

Ugumu wa maisha ndio unaongeza uhalifu,ujambazi,umalaya na hata uuzaji wa dawa za kulevya,bado naamini serikali inaweza kushughulika kwa umakini mambo haya yote.

Kila mwaka serikali imekuwa ikiongeza na kupunguza viwango vya kodi katika maeneo mbalimbali, na imekuwa ni utaratibu kwasasa kuwa kila mwaka lazima kodi ya Viburudisho pamoja na sigara ipande kitu ambacho kinafanya bei ya vitu ambavyo kodi yake inapanda kila siku kupanda sana….serikali huwa inakuwa ina majibu mepesi tu kwa hata maswali magumu.

Image

Yaani nakuwa mashakani kuhoji na kutafakari uwezo wao wa kufikiri na ubunifu wa kutafuta vyanzo vipya vya mapato kama uko sawasawa.

Maana serikali kila kukicha inaongeza matumizi lakini haitafuti vyanzo vipya vya mapato vya kueleweka…kwanza serikali yenyewe ni kubwa mno, wizara nyingi sana, maofisa wa serikali ni wengi sana wanaotumia magari ya ghali sana kuyanunua na hata kuyahudumia, safari nyingi sisizo za msingi,safari ambazo hazina matunda zaidi ya kufuja tu,misafara mirefu ya viongozi wa serikali na bado serikali inaendelea kuongeza idadi ya mikoa na wilaya na kuwa na vipao mbele dhaifu,uthibiti hafifu wa fedha za serikali na hata kama watu wakigundulika wameharibu bado wanalelewa mpaka tunasahau….SASA HAMNA NAMNA TUNAWEZA KUENDELEA KWA KUTUMIA ZAIDI YA KUZALISHA.

CHANZO KIPYA CHA KODI KIMEBUNIWA;

Mwaka huu wa fedha serikali imeongeza kodi kadhaa ikiwepo kodi ya mafuta ya taa na mawasiliano ya simu za mkononi,kitu ambacho kinaleta maumivu kwa watu wa chini kabisa….na hiyo hasara sio ya mitandao ya simu,maana na wao wameongeza gharama za mawasiliano…..zaidi eti wamebuni chanzo kipya cha mapato….”TOZO ZA KILA MWEZI KWA KILA KADI YA SIMU”…..Katika hili naona wanastahili pongezi (ikiwa uwezo wao wa kufikiri umeishia hapo),lakini siwezi kuunga mkono hata kidogo ikiwa tunaweza kufikiri kwa kina na kupata vyanzo vipya vya mapato.

Image

KODI NYINGI MNO MKONONI MWA MLALA HOI;

Haiwezekani huyu mtumiaji wa simu alipie kodi muda wa maongezi,maongezi yenyewe,huduma za kibenki za simu, huduma nyinginezo kama vile za mwito kwa akupiaye,habari na nyinginezo ambazo kuna wengi wameunganishwa na wameshindwa kujitoa hata sasa……NA SASA TUNATAKA MTU AANZE KULIPIA KADI YAKE YA SIMU KILA MWEZI….hapana huu ni uonevu.

Hivi hamuwezi kuona ni jinsi gani makampuni haya ya simu mmeyaachia pesa nyingi sana? kwanza hayasemi ukweli kuhusu uwekezaji wao na faida wanayoipata hapa nchini kwetu na hakuna ufuatiliaji wa kweli(monitoring) wa serikali…yaani mambo yanaendeshwa kienyeji tu….ujio wa huduma za kibenki kwenye simu za mkononi umeleta changamoto sana kwenye biashara ya mabenki,hususani mabenki yanajishungulisha na watu wa kawaida,zikiwemo hata zile zenye hisa za serikali.

NI VEMA KUJUA NA HAYA PIA;

Watu wanaojishulisha na uwakala wa huduma za kibenki za simu za mkononi,wanaweza kuwa wanapata faida lakini haifanani na hatari inayowakabili,maana hawana bima ya kazi hiyo….ukiwa na sehemu yako unapofanya uwakala,ikitokea majambazi wamekuvamia na kuchukua pesa zote,hiyo sio hasara ya kampuni ya simu bali wewe mwenyewe….na zaidi watu tunaoweka fedha huko,hatuna hakika saaana maana siku wakiamua kufuta kumbukumbu kwenye DATABASE yao basi tena,kwani utadai wapi?,utaenda mahakama gani na utathibitishaje kuwa ulikuwa na Milioni kwenye simu?…Kama hili ni gumu basi sawa,naamini wengi hawajapona na maumivu ya DECI hata sasa. Ieleweke kuwa sijasema hawa jamaa ni matapeli hapana,ila natamani serikali ione namna nyingine ya kufuatilia kwa karibu mambo haya…itafaa sana kama mihamala yote ingekuwa inaonekana TCRA moja kwa moja…hapo kodi na usalama fedha ungekuwa ni wa hakika,LAKINI KWA KUWA TUMEAMUA HIVYO HAMNA NENO.

VYANZO VINGINE VYA KODI;

Kuna vyanzo vingi sana vya kodi,ambavyo vikipangiliwa basi tutakuwa mbali sana,ngoja nitaje vichache tu;

1. Kwenye mipaka mingi ya nchi hii biashara ya kubadilisha fedha inafanyika kiholela tu,kwa hiyo hakuna kitu serkali inapata,maana watu hawa wanafanya biashara na fedha mkononi….mfano mzuri ni Tunduma,mpaka wa Zambia,DRC na nchi zote za kusini,ikiwepo na Afrika kusini….je ni kiasi cha kodi inapotea hapo na mipaka mingine?

2. Wajenzi/vibarua wa ujenzi waliotapakaa nchi nzima..inawezekana serikali inachukua kodi kwa makampuni ya ujenzi peke yake,lakini asilimia 90% ya nyumba za nchi hii zinajengwa na mafundi wa kawaida…na hawa hawatambuliki popote na wala hawalipi kodi yoyote…kama serikali ingeona ni namna gani inawatambua na kupata kodi kwako,naamini inatosha sana kuongeza mapato ya serikali.

Image

3. Wapangishaji wa nyumba, maduka  na fremu mbalimbali za biashara…hii ni nchi pekee ambayo hakuna uthibiti kabisa katika eneo hilo,yaani kila anajipangia kodi atakayo na kila mwaka inapanda kwa ushawishi wa madalali,tena eti wanataka kodi ya mwaka mzima…kwanini serikali haioni kama hapa pia kuna kodi? kama ukiwekwa utaratibu unaoeleweka wa wapangishaji kulipa kodi pamoja na madalali,naamini pia ni chanzo cha uhakika kabisa cha kodi.

4. Kazi za Sanaa…ingawa serikali inaleta mpango wa kuweka stika za kodi kwa kazi za sanaa,lakini bado naona hakuna mkazo sana maana imewekwa kama hiari ya msanii mwenye kazi hiyo,lakini laiti ikiwa ni sheria kuwa kila CD/DVD ama kazi yeyote ya sanaa ilipe kodi,pamoja na hizi filamu toka nje ya nchi,hususani hizi filamu zinazokuwa nyingi ndani ya moja ,nina uhakika Sanaa ya ndani ingeheshimika,wasanii wangeneemeka na serikali ingepata mapato ya kutosha.

HIVI NI VICHACHE TU KATI YA VILE AMBAVYO SERIKALI INAWEZA KUVIFIKIA  NA KUVIFANYIA KAZI,LAKINI ZAIDI KAMA SERIKALI INGESIKILIZA KILIO CHA WATANZANIA CHA MUDA MREFU CHA KUREKEBISHA KODI KWA MAKAMPUNI YA MUCHIMBA MADINI PAMOJA KURUDISHA KODI MBALIMBALI ZILIZOFUTWA,IKIWEMO KODI YA UINGIZAJI WA VIPURI NA MAKEMIKALI YA KUCHIMBIA MADINI; KODI ZA MAKAMPUNI YA UTALII NA MAHOTELI, NINAAMINI SERIKALI ITAKUWA NA FEDHA NYINGI SANA ZA KUTUMIA.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI;

1. Lazima itafute timu ya watu wanaoweza kufikiri na kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa faida ya kesho ya Tanzania

2. Serikali ipunguze matumizi ya kawaida na kuongeza uwekezaji wa ndani; fedha ifanye maendeleo sio iishe kwa matumizi ya kawaida na mishahara.

3. Serikali iongeze uthibiti wa mapato hayo yanayopatikana hata kama ni kidogo,maana haina maana kuwatesa wananchi na bado serikali inawafuga mchwa wanaotafuna na kufuja pesa za walipa kodi.

4. Serikali lazima iwapende wanachi wake,kwa kuweka kodi kubwa sana vitu kutoka nje kuingia ndani na hayo makampuni makubwa ya uwekezaji na kupunguza mzigo wa kodi wa wananchi wa kawaida….zaidi serikali iache dharau,haiwezekani JKT watengeneze fanicha lakini yenyewe iagize fanicha za serikali nje ya nchi.

5. Ipunguze matumizi yasiyo ya lazima kwa kutoa mitaji kwa baadhi ya taasisi zake ili zijiendeshe zenyewe….mimi ninaamini JKT na MAGEREZA vinaweza kujiendesha na kujitosheleza kama wakiwepo watu makini na kama serikali ikijidhatiti kweli.

MWISHO;

Binafsi bado ninaamini kuwa ipo nafasi ya kujirekebisha, haiwezekani nchi hii iendeshwe kwa “DHARULA” katika kila eneo…yaani Umeme dharula,Elimu Dharula,sasa imekuwa ni kama utaratibu vile,haiwezekani kukurupuka tu katika kila jambo…mambo mengi kwenye nchi hii yanaenda kama vile hamna wasomi ati,Wakati amekuja Obama ndio niligundua uzembe mwingi sana,lakini leo sisemi lolote hapa,ila lazima ijulikane kuwa Wazalendo bado tupo wengi sana na tunaamini serikali inasikia maoni ya wananchi bila hila,hivyo kwa niaba ya wanachi naomba na yangu myafanyie kazi….Msione wananchi wana line mbili na kuendelea mkadhani labda maisha ni mazuri sana,hapana,ni kuwa mtu anajaribu kupunguza gharama kwa kupiga watu wa mtandao huu kwa kadi husika na ule vile vile. Wasomi nchi hii bado hawajaheshika wala kutumiwa vema.

Pamoja na yote yanayoendelea katika nchi, bado ninaipenda nchi yangu na kamwe sitoacha kuipenda maana nilizaliwa hapa kwa kusudi maalum,naam mpaka kusudi hilo litakapotimilika ndio nami nitapumzika katika maisha haya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA NA WATU WAKE WOTE, AMEN!

Na. CHAVALA, FREDY E.

+255 713 88 37 97

…….TATIZO LENU MNAYAACHA YALE MEMA NA KUYASHIKILIA YA KIJINGA!!!!(Mwl.J.K.Nyerere)

Image

Afrika ni bara zuri sana na ni la pekee duniani!

Afrika ina utajiri wa kuweza kuifanya dunia nzima mahali pazuri pa kuishi,ila tatizo ni ubinafsi,uvivu na ukengeufu wa wengi wa waafrika!

Wachache waliobatika kupata mwanga wa elimu na yamkini kushika baadhi ya nafasi za uongozi katika ngazi mbalimbali,wameshindwa kutumia nafasi hizo kuwajulisha wengine haki zao,ila kinyume chake wametumia ujinga wa watu wao kuwaonea na kuwanyonya kabisa!

Viongozi waasisi wa afrika sio kwamba walifanya makubwa saana ila kwa yale walioyaanzisha kama yangetiliwa mkazo na kuendelezwa ipasavyo naamini tungekuwa mbali zaidi mara 10 ya hapa tulipo sasa.

Na ndio ninashawishika kuuzungumzia sehemu kidogo ya hotuba ya nyerere akiwa hai (Samahani ninakuletea nukuu isiyo rasmi)

Alisema”………Viongozi waliopita wamefanya mema yao na mabaya yao,na wanaofuata pia vivyo hivyo, na kiongozi yeyote anayefuata baada ya kiongozi mwingine anawajibika kuendeleza yale mema na kufanya yake mema zaidi na kuachana na yale ya kijinga….ila TATIZO LENU NINYI MNAYAACHA YALE MEMA NA KUYAFUATA YA KIJINGA..hahahahah”

Na kweli ukizingatia utagundua ukweli wa maneno haya….hotuba zake zimejaa kibao lakini siamini kama viongozi wetu wengi wanazielewa….vivyo hivyo na mahali pengine afrika naamini hatukuwaelewa waasisi na ndio maana tunayaacha mema na kuyafuata ya kijinga…Kwa mfano nyerere amewahi kusema madini tusichimbe kwanza mpaka tutakapokuwa na uelewa na ufahamu wa kutosha kuchimba na kunufaika sisi wenyewe,lakini kinyume chake ni kuwa mara alipokufa tu basi tukayaacha yale mema yote na kuyafuata ya kijinga!!

Kuna vitabu vyake kadhaa ambavyo vimepotezwa kiajabu ajabu, yamkini kama watu wangesoma vitabu hivyo labda amani hii isingetutosha!

Kwasasa tuna utulivu rehani ambayo bado tunaiita amani na viongozi bado hawasomi nyakati kuwa watu sasa wamechoka na maisha yao na siasa inakaribia kupoteza mashiko kwa muegemeo wa serikali!!

Naamini bado tunayo nafasi ya kuwaelewa viongozi hawa na kuleta mabadiliko ya kweli…kama tukiamua kufumbua macho na kuyatolea uvivu madudu yote katika Bara letu la Afrika na hususani nchini kwetu Tanzania hakika heshima yetu haitafutika katika vizazi vyote vitavyokaka juu ya bara hili!

Mungu ibariki Afrika,Mungu Ibariki Tanzania

Amen!

In Life you can…

In Life you can either be a SETTLER or a PIONEER. Settlers are comfortable with the way things are. They’ve stopped taking risks. They mark themselves ‘present’ in life’s attendance book but are ‘absent’ in life’s achievement register. But PIONEERS take on NEW CHALLENGES. They are TRAILBLAZERS and EXPLORERS! The spirit of a PIONEER rests upon you. You cannot be held down. YOU ARE A BARRIER BREAKER!!!

Dr.Mensah Otabil-Ghana

MORSI OF EGYPT HAS NOW EXPIRED IN PEOPLE’S HEART!!!

morsi-egypt.jpg

The crowds on the street in Egypt over the past days have been overwhelming—they have numbered in the millions. Waving flags and tooting whistles, trumpeting vuvuzelas, drumming and shouting and chanting and honking and singing—Tahrir reached such a noisy level of jubilation that people were joking, “Did Egypt win the World Cup?” Walking among them, dodging fireworks, it felt upside down: a popular protest to oust President Mohammed Morsi, the Muslim Brotherhood leader who was democratically elected, in which, since Monday, the military has taken the side of the protesters. From one perspective, what is happening in Egypt represents an extraordinary repudiation of political Islam. From another, it is an outright military coup—a repudiation of the process of politics itself. Whatever the air of joyousness, dozens of people have died across the country. The danger did not dissipate with the announcement by the military, on Wednesday night, that Morsi was not President any longer and that the Constitution had been suspended.

The crowd in Tahrir has been varied: families, including women; people with prayer calluses and Afros, some wearing plastic sandals and others Gucci sunglasses; farmers and accountants. But there’s no doubt that there are many from the middle-class “couch party”: people who were more or less O.K. with Mubarak, who tend to trust the Army, and who had not been out to protest before. Police were hoisted onto shoulders. Overhead, military helicopters dropped flags for the cheering masses. On TV—the military had taken control of state media—aerial footage of the immense throngs played on a loop to a soundtrack of martial victory music.

On Monday, Abdul-Fattah el-Sisi, the Head of the Supreme Council of the Armed Forces, issued an ultimatum: the two sides, government and opposition, had forty-eight hours to come up with a compromise plan or else the military would step in with its own “roadmap.” The crowds on the street went wild, taking it as a sign that they had already won. But this was also very clearly a coup. (Twitter captured the national sense of humor—only Egyptians could announce a coup forty-eight hours in advance!) As much as the generals say they are honoring the will of the people, they engineered a showdown, and got one. The Muslim Brotherhood’s supporters, if outnumbered, were also gathering in the streets. Among the anti-Morsi crowds that kept coming, to fill practically every square and intersection in the country, people seemed to think that the Army was not like it had been before, that it was not the Army of Hosni Mubarak and military trials. Sisi would not “sit on the chair”—that is, take the throne.

Morsi addressed the nation at 11:30 P.M. on Tuesday. He spoke with passion, sometimes with anger, and he was defiant. He used the word “legitimacy” so many times that it began to sound like a fist thumping on the table. He reiterated that he was democratically elected—and that was that. It was the feloul, he said, the remnants of the old régime and the deep state, who were taking advantage of the protests for their own schemes. He complained that the bad economy—a major complaint against him—was the fault of the previous government. He might have been right about all of that. But he did not directly address the public’s grievances, other than with a brief aside about a possible reconciliation committee or amendments to the Constitution and getting the youth involved. None of that was new: the opposition—itself fractious and divided—has thrown up its hands at these kind of pluralistic assurances. He did not mention the protests. It was as if he was living in a parallel universe, shut in a room where his own arguments bounced off the walls and echoed back to him.

I remember attending demonstrations last December outside the Presidential Palace which were organized to protest a unilateral declaration by Morsi that paved the way for the Brotherhood to ram through a contentious Constitution. Morsi has admitted that he made mistakes over the past year. But Egyptians are also reacting to the tone and tenor of his administration, which has been high handed: trying to close shops at 10 P.M. because people should be fresh for the morning prayer (Cairo is the city that never sleeps, where there are still traffic jams at 2 A.M., and where Internet usage peaks at 12.45 A.M.); prosecuting journalists for insulting the President; calling people who don’t agree “infidels.” Little legislation has passed. And everywhere there is concern about the weakness of the economy. This is what is uniting the forces of youth and revolution, feloul remnants, Christians, Army and police officers, and the middle class. The crowds turned on the Brotherhood with the cry: “Erhal!” (“Leave!”)

But across the river at Cairo University, another vast crowd, not as big but certainly numbering in the hundreds of thousands, was equally jubilant and staunch in its support for Morsi. Morsi’s only option, shorn of control over the police and the Army, was to get his people onto the streets in response. Guns were appearing on the edges of the crowd and at 2 A.M. I got a text from a friend on the streets: “It’s happening! Semi-automatics everywhere!”

The approach of the deadline on Wednesday brought a rash of rumors: senior Brotherhood members had been placed under travel bans, the Army had dictated a headline to the state newspaper calling for resignation, the bodyguards of the Brotherhood’s Supreme Guide had been arrested. When I visited the pro-Morsi rally in Nasr City this afternoon, the atmosphere was impassioned and worried. The men I talked to (I saw only three women in an hour there) were very careful not to criticize the Army, but their trepidation seemed only to belie their desperation. “Tell people to come out and support us!” one man said, almost plaintively. Many were wearing crash helmets and swinging bamboo sticks, but they were friendly, shielding me with an umbrella against the sun. “This is the last moment to save our Islamic project” one man told me. Others talked about fighting for democracy. Another said, “Do you know what its like to stand here all alone, with no one beside you?” As we talked, the Army convened a meeting of different political parties to which the Brotherhood refused to attend.

An hour later I was in Tahrir Square when a giant cheer went up at an unconfirmed rumor that Morsi had been put under house arrest. They cheered the tanks in the streets, too, and, after nightfall, there was utter jubilation as Sisi came on television to announce that the Morsi administration had come to an end. Adly Mansour, the head of the Supreme Constitutional Court, would be Egypt’s interim leader. The public didn’t know where Morsi was or what the Brotherhood would do. As I walked through the crowd in Tahrir, I could still see the old scrim of anti-military graffiti from a year ago, underneath the portraits of new martyrs.

Photograph by Khaled Desouki/AFP/Getty.